HOME

PROVERBS

CUISINE

TARAAB

MASHAIRI

DUA

RIDDLES

PICTURES

TARAAB LYRICS

SUPERSTITIONS

VISA NA MIKASA

MUSIC

ARTICLES

QASWEEDA

1      Twakuomba mtukufu.
        Asokijana na kufu.
        Mola wetu maarufu.
        AlIahu alo karima.

2      Mikono tumeinua.
        Mola wetu watujuwa,
        Takabali yetu duwa.
        Utupe lililo nawema.

3      Mola machozi yatoka.
        Hakika ya bubujika,
        Tumetubu kwa hakika.
        Waja wako tumekoma.

4      Rabbi sisi waja wako.
        Twatubu twa rudi kwako.
        Tutini ya twaa yako.
        Tukubaile karima.

5      Ya Rabbi tupe Ilimu.
        Tupe na njema Fahamu.
        Ya kutambua vigumu.
        Vya dini yako Karima.

6      Utupe matunda yake,
        Tuisome tusichoke.
        Mola ilimu iweke.
        Moyoni mahala pema

7      Rabbi ijapo hukumu.
        Isiwe kwetu ni ngumu,
        Tusiweze kudhulumu.
        Tukuche wewe Karima.

8      Turuzuku nyingi hima
        Isiokuwa na kukoma.
        Utupe na kulla jema.
        Duniani na kiama.

9      Tupe Riziki halali.
        iso na uthakili.
        Utupe na njema hali
        Duniyani na kiyama.

10     Tuondoshee laudhiya.
        Lilo na kulla baliya,
        Utupe liso udhiya.
        La-dini yako karima.

11     Utupe na kupendana.
        Sisi na wetu vijana,
        Mapenzi yaso khiyana.
        Ya dini yako karima.

12     Utupe njema fasaha
        iso kuwa najaraha.
        Utupe nyingi furaha,
        Duniani na kiyama.

13     Tutunze mijini mwetu.
        Tukidhie deni zetu.
        Kabla ya kuja kwetu,
        Mjumbe wa mauti mwema.

14     Sizi vunde zetu hima,
        Tuawini wima wima.
        Utujaze yako mema.
        Duniani na Kiyama.

15     Tubarikie Jalili.
        Umriwetu twawili.
        Sote na kulia adili.
        Afunzae kula jema.

16     Kulla ajae na shari.
        Waijuwa yake siri
        ivunde yake dhamiri.
        Asiweze kusimama.

17     Rabbi swala na salamu.
        Umfikilie hashimu
        Na sahaba ze kiramu
        Na alo kulla mwema

18     Amina Rabbi Amina
        Amina Rabbi Amina
        Amina Rabbi Amina.
        Tukubalie Karima.