HOME

PROVERBS

CUISINE

TARAAB

MASHAIRI

DUA

RIDDLES

PICTURES

TARAAB LYRICS

SUPERSTITIONS

VISA NA MIKASA

MUSIC

ARTICLES

QASWEEDA

 

Mama nieleke. (KITANDA)    Mother! Carry me on your back. (BEDSTEAD)

Parr! Hata Makka. (UTELEZI) Prr! straight to Mecca. (SLIPPERINESS

Nende huko na nikirudi nimshike Ngombe wa mama mkia. (KATA YA MAJI)  Let me go far away and when I come back let me catch hold of the tail of my mother’s cow. (LADLE for DRINKING WATER)

Nyumba yangu haina milango.(YAI)   My house has no door. (EGG)

Kitendawili changu cha ajabu kina matone ya dhahabu. (QURANI TAKATIFU) My wonderful riddle is adorned with spots of gold. (THE HOLY QURAN )

Ubwabwa wa mwana mtamu. (USINGIZI)  A child's porridge is delicious. (SLEEP)

Kipo lakini hukioni(KISOGO) It is here but you cannot see it(THE NAPE OF THE NECK)

Nilikuwa nikienda njiani nilipomsikia mtu akinita  Wifi! Wifi!” lakini nilipogeuka sikumwona mtu. (MBAAZI KAVU)        I was going along the road when I heard a person calling me, Sister -in-law!’but when l turned round there was no one    in sight. (DRY PIGEON-PEAS in THEIR PODS)

 


Nzi hatui juu ya damu ya simba. (MOTO)
The fly cannot settle on the lion’s blood. (FIRE)

Bibi mweupe ametupwa mibani. (MACHICHA YA NAZI)
The white lady has been thrown upon the thorns. (THE SHREDS OF THE MEAT OF THE COCONUT AFTER THE MiLK HAS BEEN SQUEEZED OUT OF IT)

Pana visu vingi lakini mpini mmoja tu. (CHANA YA NDIZI)
There are many knives but only one handle.(A BUNCH OF BANANAS)

Ukiona Njigi’ utadhani ‘Njege’; na unapoona Njege’ utafikiri ‘Njigi’. (MAZIWA NA TUI LA NAZI)
If you see ‘Njigi’ you will take it be Njege’;and should you see Njege’ you will ihink it Njigi (COW-MILK AND COCONUT-MILK)

Popoo mbili zavuka mto. (MACHO)
Two areca-nuts cross a river. (EYES)


Nyumba yangu ndogo ina madirisha mengi.(DEMA)
My house is small but it has many windows. (A FISH- TRAP)

Kombe Ia Mungu Ii wazi (KISIMA)
God’s cup is open. (A WELL)


Nimewafungia milango wanangu huku wakipigana
(BISI ZIKIKAANGWA)
I have shut the door on my children and they
are now fighting. (MAIZE-SEEDS BEING
ROASTED)
Nyumba yang kuu ina mlango mdogo.
(CHUPA) 
My house is large but its door is small. 
(BOTTLE)
Wanangu wote wamevaa vizibao, wasiovaa si
Wanangu. (KUNGURU WENYE MABAKA MEUPE)
My sons wear Waistcoats: those who do not are
not my Sons. (WHITE-BREASTED CR0WS) 
Nimeanika mpunga wangu juani lakin, kulipopambazuka
sikuuona. (NYOTA)
I have put my paddy rice in the sun to dry but
when day dawned I couldn’t see it. (STARS)

Watoto wangu wote wamevaa kofia, wasiovaa si
wanangu. (FUU)
All my children have caps on. those without
are not my children. (FRUIT OF VITEX CUNEATA )

Nina watoto wanne, lakini akiondoka mmoja
waliosalia hawafanyi kazi. (MATENDEGU YA
KITANDA)
My children are four in number but, when one
goes away, the rest cannot work. (THE LEGS
OF A BED)