HOME

PROVERBS

CUISINE

TARAAB

MASHAIRI

DUA

RIDDLES

PICTURES

TARAAB LYRICS

SUPERSTITIONS

VISA NA MIKASA

MUSIC

ARTICLES

QASWEEDA

      TAANASI NA MAPOKEZI YA KALE YA WA-MVITA

               Na Ahmed Hussein Ahmed, B.A. , M.A., Dip. Ar.

             

         TAQADIMU

        

         Mapokezi ya kale ya wa-mvita’ yaliweza kuchukua sehemu moja ya Fasihi simulizi ambayo   ilitumbuiza, nasihi, taanasi, sherehesha, kutoa taazia na kwa malengo mengineyo.   Maarufu zaidi katika mapokezi hayo ni matumbuizo ya watoto wakati wa faragha (mapumziko) na   wanapojianda kwenda kulala          Wazee wa kale wa Kiswahili walikuwa na namna nyingi za kuwatumbuiza watoto wao. Kati ya   namna hizo ni kuwaimbia vipokeo, kuwatolea hadithi, mashairi na nyimbo mbali mbali nyakati za   jioni Wakati mwengine watoto na vijana wa marika mamoja wanapopata nyakati za faragha    hujitumbuiza kwa vipokeo na michezo kadha wa kadha        

         Makala haya yatahusisha baadhi ya mapokezi hayo 2. Mkazo zaidi utatiwa katika mapokezi ya   watoto na vijana wa kimvita Msomaji apaswa kufahamu kuwa mapokezi kama haya huweza pia   kupatikana katika sehemu nyengine za Afrika mashariki na pengine janibu ya sehemu hizo.

        

                    UKALE WA MAPOKEZI

 Bado hakujajulikana ukale hasa wa mapokezi haya. Kulinganana baadhi ya mapokezi   yanatufanya tutoe makisio fulani juu ya tarehe ya mapokezi hayo. Kwa mfano        

                                    “Peepepepeta

                               Wazungu wawili wapita

                                 Wan ‘kovu za kitwa

                                Wakitoneshana wateta

                              Sara n’tokapi na ulingo

                             ‘toka n'komani Baulingo..." 

        Mapokezi haya yanakisika kuwepo tokea karne ya kumi na tano ambapo wareno na wazungu   wengineo walikuwa wameshawasili sehemu za Mvita. Halikadhalika, kutajwa kwa neno "shilingi"   inatueleza kuwepo kwa matumizi ya sarafu katika kame kumi na nane au pengine kabla yake.           Mfano wa mapokezi yenye kutumia neno hilo Ia sarafu tulilo nukuu hapo juu ni huu ufwatao:

            "Shilingi yangara yaua (kipokezi hurudiwa mara mbili),

               sijauona mpili pili  na maua yake mchikichoo...."        

  Yaamkinika pia ,baadhi ya mapokezi haya ni ya jadi najadi Katika baaadhi ya sababu   zinazotufanya tudhanie hivyo ni kule kuwepo kwa istilahi za kale na/au zilizo sahaulika3.         

          MAUDHUI NA MALENGO YA MAPOKEZI        

 Mapokezi ya watu wa kale yalikuwa na malengo na maudhui mbalimbali. Yapo yaliyodhamiriwa   kutumbuiza, kufunza vijana, kuwashajiisha,na kuwaongoza wawe ni watoto wema wenye  nidhamu. Mapokezi haya yalitumika nyakati za kupasha jando, harusi, mavuno na wakati wa huzuni na misukosuko.       

 ‘Kisiwa cha Mvita sasa chafahamika zaidi kwa jina Ia ‘Mombasa’ Hapa ndipo mahali mwandishi alipozaliwa na alipokulia.  Maandishi mengi ya kale yametumia neno ‘Mvita’ kuliko jina lenginelo. Hii ni moja ya sababa muandishi amependelea kutumia  jina hilo katika makala haya. Natoashukurani nyingi kwa dadaangu Bi. Leyla Ali Abdalla (b. 1962) wa Magongo, Mombasa, ambaye alitumia wakati wake   mrefu kunisimuliya na kunitolea kimahadhi baadbi ya mapokezi haya, 10 Desemba, 1998.. 3 Mahojiano yangu na mzee wangu Shelkh Ahmad Nabahany, mtafiti mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, Mombasa, Swahili   Cultural Centre 21 May,1998.

           MAPOKEZI YA WATOTO NA MICHEZO YAO        

         Watoto na vijana hujumuika pamoja kwa matumbuizo na taanasi mbali mbali hususan nyakati za  jioni Mara nyengine katika sherehe rasmi, wakunga na wavyele hukusanyika kuwaongoza vijana   hasa wanaobaleghe na wanaokaribia kufunga ndoa

         Michezo marufu ya watoto wa Kiswahili tangu zama hizo ni pamoja na kucheza kibe ndolee,   ulimbo, tega n'kutege, blada, nusu mkalili, kuruka kamba, Kurusha tiara,mieleka, kirumbizi, kupiga   goma (ya ropa), na michezo mengineyo. Nyakati nyigine wavyele wanapopata faragha  huwatumbuiza watoto wao kwa qasida, mashairi, haditbi, vitendawili na mapokezi mbali mbali.  Yafuatayo m baadhi ya mapokezi hayo:       

                                  Bibi songa nyele        

                          Bibi songa nyele shanuo la nini?

                            Kitwa chaniuma dawa yake nini?

                           Ponda tangawizi upake nyusini,

                            Mahaba sindano ya choma maini       

        

                                      Aliyomi        

                         Al yomi aliyomi alimsabaha ilyomi,

                        Kuna mnazi mmoja wapanda watu watatu

                        Akianguka mmoja, Hamadi mwana wa watu.

                        Ndege ruka ndege ruka na barua mdomoni

                         Ukufika ukafika mbwagie mapajani.

                      Usinione nimekonda ukadhani kwetu sili

                      Nala mtele kibaba na nyama nusu ratili

                              Kitoria baa kitoria baa

                              Kahela kahela kajumbaka.

                                        Pepeta

                                     Peepepepeta

                               Wazungu wawili wapita

                                 Wan ‘kovu za kitwa

                                Wakitoneshana wateta

                             Sara n n'tokapi na ulingo

                            Natoka mkomani kunwa tembo

                             Kesho n'tashuka Marekebu

                            Na zinga lamoto Ia dhahabu.

                             Sukuma kidau tunende

                              Kwa Bwana Hamadi Madende

                                Tukampokonye maembe

                              Na wali mtamu kwa tende

           Mariamu na mpishi wake (Kipokezi hiki hurudiwa mara mbili).

                                     Ukuti wa mnazi

                                      Ukuti ukuti

                                 Wa mnazi wa mnazi

                                   Ukingia upepo

                              Wan ‘tetema Wan ‘tetema

                           Msegeju

                                 Msegeju ana ngombe

                                 Nami n ‘no ngombe zangu

                                Namwambia tutanganye

                                  Hataki

                                  Kwa heri nenda zangu.

                                    Mapokezi ya Harusini

                                       Bibi harusi ndoo kaole

                                       Kaole mgeni kangia

                                       Mgeni kongo

                                       Aya eei    Mgeni kangia.

                                         Hongera mwanangu ee

                                        Hongera nami nihongere mwana eei

                                       Mama uchungu mwana uchungu

                                        Eei

                            Nyamala mwonangu siliye oyee

                          Tumbo la uvyere linaumo mno eei

                                 Linauma mno hoyee!

        

                         Sema yuwapi mamake harusi aje hapa

                             Tuhangaike naye (kipokezi)

                           Na ndugu yake harusi aje hapa

                            Tuhangaike naye

                            Na rafiki yake harusi aje hapa

                            tuhangaike naye...

                            Aje amfunze mwari

                            Asije kufedheheka

                            Amwitikie mumewe kwa kila anachotaka.. 4

                

                   Mapokezi yanayotolewa na tanaasi

           Yapo mapokezi ambayo watoto wa mvita huyatowa huka wakitaanasi u kucheza michezo mbali   mbali. Baadhi ya taanasi hizo m michezo mbaiimbaii nayo huchezwa hivi:         

                      4Rajiisha maelezo ya nambari 2 (mbili) hapo juu.

                             Ulimbo

  Katika ulimbo wasichana hufanya mviringo wakishikana mikono. Binti yeyote hutajwa na kuingia  kati kati ya boma akicheza kwa maringo huku akiimbiwa

                                 Ulimbo bayoyo baa

                           Binti fulani piga goti tukuone

                            Bingili bingili mpaka pwani        

                 Barua kwa baba        

         Kijana hushika barua au mfano wake na kuzunguka nje ya boma Ia waliokaa chini huku akiimba  “Napeleka barua kwa baba”. Kijana huyo atazunguka huku akilenga mtu wake kimoyomoyo.

  Anapomkaribia atamgusa na huku akitimka mbio. Aliyeguswa naye atamfurusha huyo mwenye  barua hadi amshike. Akishindwa kumshika mwenye barua basi alochukua yeye barua na kufanya   kama mwenye barua wa kwanza alivyofanya. Mwenye barua huimba mapokezi yake hivi:

         

          Napeleka barua kwa baba, ikanipotea ndiani(Hurudiwa mara mbili)

         Si wewe, na si wewe, ni wewe... (mwenye barua akifanya uchaguzi wake).         

         Kipara ngoto

         Anaye nyoa nyele (kipara) hugolewa na wenzake na kuimbiwa:

        

                             Kipara ngoto, maji yamoto

                                Ukimpata mtie ngoto.

        

         Kidengele

         Anaye onaekana na kitu chepesi kama vile sufi au unyoa utosini mwake pasi na yeye mwenyewe  kujitambua, hugolewa na wenzake na kuuimbiwa:

                              Mtu wangu an ‘kidengele

                               Kesho ‘tam nyoa nyele.

        

         Matezo ya simba

         Katika mchezo huu mmoja wa wanadi katika vijana atajifinya ni baba anaye nadi  kuwatahadharisha watoto wake juu ya udhalimu na uvamizi wa simba. Mnadi huyo kumbe   nimvamizi pia. Hivyo basi atanadi na wenziwe kumuitikia mnadi anapofika pale kwenye msemo  usemao ‘nashuka chini ‘mnadi ataruka na kuwatimua mbio vijana wenziwe hadi amshike mmoja   wao. Mapokezi ya ‘matezo ya simba’ ni haya yafuatayo:        

         Mnadi:    Watoto wangu eeh!

         Wapokezi: Eeeh!

         Mnadi:    Mimi baba yenu

         Wapokezi: Eeeh!

         Mnadi:Sina nguvu tena eee ya kuua simba.

         Wapokezi: Eeeh!

         Mnadi:Simba m mkali eeh!

         Wapokezi: Eeeh!

         Mnadi:Aliua mama eels!, akaua nyanya eels!, akaua ndugu eels! akaua...

         Wapokezi: Eeeh!

         Mnadi:    Nani kamata?

         Wapokezi’Mimi kamata, kama mume kweli kama mke kweli sishuka chini

        Mnadi:     Haya nashuka chini(Mnadi ataruka na kuanza kuwatimuwa mbio wenzake hadi amshike  mmoja wao).        

                                               Kizuizui

                   Mchezaji hufungwa macho (kizui zui) zw) kwa lengo Ia kushika mtu katika kundi la wachezaji   wenziwe. Anaye shikwa naye atafunga kizuizui 5.

                           Mpunga na nyama na uliwe

                   Mpunga na nyama na uliwe ni mchezo ambao vijana hukusanya mlima wa mchanga na kijiti  Kikawe kwa juu yake. Wachezaji huwa wawili au watatu. Kila mmoja huvuta mchanga   polepole  upande wake kwa vidole vya mikono miwili hadi kijiti kianguke upande wa mshindi

                            Haliya  totore

    Wale wanaoshindwa katika michezo mwisho huimbiwa        

       Waliyataka wenyewe, haliya totore.  ilobaki n ‘shauri yao               

                   Ngoma

             Zifuatazo ni baadhi ya ama ya ngoma maarufu zilizokuwa zikipigwa kisiwani Mvita hadi kufikia  wakati wa uhuru 1963 Ngoma hizo za kale zilizosifika ni Kirumbizi, Twari la Ndia, Vugo7 Lele   mama, Chakacha Mdodoki, sengenya Kimanyema Mabumbumbu, Namba, Gwaride, Twarabu,              Sumsumiya, Mwaribe, Sindimba, na Mwanzele.       

         Ngoma chache mno bado zingaliko kisiwani Mombasa pindi makala haya yalipotayarishwa na mwandishi. Baadhi ya ngoma tulizonukuu hapo juu zimekufa baada kukemewa na kupingwa na mashekhe na wanazuoni Afrika  Mshariki        

         TAKHATIMU

         Makala haya yamejaribu kwa kiasi fulani kutoa maelezo juu ya mapokezi na taanasi mbali mbali za wa-Mvita.  Mapokezi haya ambayo yanakaribia kutoweka na mengine kusahaulika kabisa yaliweza kutumbuiza, kuongoza,  kufunza, kushajiisba, kufurahisha na kuhuzunisha hadhirina mbalimbali. Mapokezi haya yaliweza pia kujenga  maadili, dasturi na adabu za watoto wa Kiswahili. Fasihi simulizi kama hii iliongeza ladha utamu wa lugha na   kukipamba Kiswahili Hapo ndipo tukasema ‘kila msimu ukija huja na yake’        

                   Haki za kunakili ni za c- Ahmed Hussein Ahmed 

                          5 Mahojiano yangu na Sheikh Mohammad AbdulRahman (b. 1940), Mombasa, 28th May 1998. Halikadhalika, natoa shukurani  kwake na kwa wengine ambao sikuwataja hapa kwa usaidizi wao walionipa katika kukusanya na kuziandika baadhi ya mapokezi   na taanasi za wa-Mvita.  6 Rajiisha namba 5 (tano) hapo juu.  7 Ngoma ya ‘vugo’ bado ingali maarufu upande wa Lamu na Siyu